Wanafunzi 1, 392 wa shule ya msingi bukaga iliyopo wilaya ya nyamagana mkoani mwanza wapo hatarini kukumbwa na ugonjwa wa kipindupindu baada ya kinyesi kutapakaa ovyio kwenye maeneo yanayozunguka shule hiyo kutokana na uhaba wa matundu ya vyoo.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo Rose Masebu amesema shule yake inazo changamoto nyingi zinazoikabili kwa kipindi kirefu, ikiwemo uhaba wa walimu, ofisi, madawati, vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo ambayo hivi sasa yamejaa na kusababisha kinyesi kuanza kutapakaa,hali ambayo inaweza kusababisha kuibuka kwa magonjwa ya milipuko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha, huku serikali ikilaumiwa kwa kushindwa kuzitafutia ufumbuzi changamoto hizo.
Kwa upande wao baadhi ya wakazi wa kata ya kishiri ,waliozungumza wameeleza kusikitishwa na mazingira duni ya shule hiyo, ambapo wameiomba serikali kujenga matundu ya vyoo vitakavyotosheleza mahitaji ya wanafunzi zaidi ya 1300 wa shule hiyo ambao kwa hivi sasa wanalazimika kutumia matundu manne tu, ambayo hayakidhi mahitaji yao.
Uchunguzi katika shule hiyo umebaini kuwa wanafunzi wengi wanakalia mawe na matofali wakati wa vipindi darasani kutokana na uhaba wa madawati, lakini pia ofisi za walimu nazo ziko hoi taabani kwani hazina samani, hali hii inasababisha walimu kujikuta wakifanya kazi zao katika mazingira magumu, kama anavyoeleza mwalimu Naomi James.
shimo la choo lililochimbwa kwa michango ya wazazi sasa lina miaka minne bila kujengewa, je halmashauri ya jiji la mwanza imejipanga vipi kuwanusuru wanafunzi hao 1,392 ili wasipatwe na magonjwa ya milipuko ? .Hilo ni moja ya swali nimejaribu kujiuliza kutokana na hali ilivyo huku je wahusika mnachukua jukumu gani kumaliza hili.
No comments:
Post a Comment