Monday, 20 April 2015

YALIYOJIRI DAR LIVE KATIKA SHEREHE YA WAUZA MAGAZETI


Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers Ltd, Eric Shigongo, akisalimiana na baadhi ya wauza magazeti  baada ya kuwasili Dar Live
Pichani kutoka kulia ni Katibu wa Mawakala na Wauza Magazeti, Msokolo,  wa pili ni mwenyekiti wake, Mzee Deo, katikati ni Eric Shigongo,  akiwa na Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho na Afisa Utawala wa Global Publishers, Soud Kivea
Mkuu wa Idara ya Usambazaji, Lawrence Kabende,  akiwatambulisha viongozi.(P.T)
Mmoja wa wauza magazeti jijini akichangia mawazo yake katika sherehe hiyo
Mwenyekiti wa mawakala, Mzee Mdoe, akizungumza na wauza magazeti
Eric Shigongo akizungumza na wauza magazeti
Baadhi ya wauza magazeti wakiwasikiliza kwa makini viongozi wao
Muda wa maakuli! Mhariri wa gazeti la Ijumaa Wikienda, Sifael Paul akiongoza foleni ya chakula, akifuatiwa na Mhariri wa gazeti la Risasi Jumamosi, Erick Evarist
Mmoja wa wauza magazeti ajulikanaye kama ‘Black Commando’ akionesha uwezo wa kuimba jukwaani
Wafanyakazi wa kampuni ya Global Publishers ambao pia ni wanamuziki wakilishambulia jukwaa.  Kutoka kushoto ni Benjamin Mwanambuu na Deogratius Mongela
Msanii wa kizazi kipya, Y Tony akiimba kwa hisia
Kundi la wanaume Halisi likiongozwa na Juma Nature (wa kwanza kulia) wakikamua
WAUZA magazeti wa Mkoa wa Dar es Salaam jana walipata fursa ya kusherehekea miaka 17 ya kampuni ya uchapishaji magazeti ya Global Publishers Ltd katika tafrija iliyofanyika Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live, Mbagala-Zakhem.
Sherehe hiyo iliyohudhuriwa na mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers Ltd, Eric Shigongo, ilikuwa na fursa ya kubadilishana mawazo kuhusu changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wauza magazeti na kujiwekea malengo mapya katika mwaka huu wa mauzo.
(Picha na Deogratius Mongela na Chande Abdallah/GPL)

Tuma Maoni

No comments: