Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania JWTZ kurugenzi ya mawasiliano imedhibitidha kuuwawa askari wake wawili waliokuwa wanatekeleza jukumu la amani katika nchi ya kidemokrasia ya kongo DRC.
Katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salam kaimu msemaji wa jeshi hilo Meja Joseph Masanja amesema wanajeshi hao wamefariki dunia usiku wa tarehe tano baada ya msafara wao kuvamiwa na kikundi kinachosadikiwa kuwa ni cha waasi wa ADF wakiwa katika mji wa mavivi.
Meja Masanja amesema katika shambulio hilo la silaha gari ambalo walikuwepo askari hao liliteketezwa kabisa na hivyo kupelekea vifo vyao na askari wengine kumi na sita kujeruhiwa ambapo mpaka sasa wanapatiwa matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.
Askari hao ni miongoni mwa askari 46 waliyokuwa katika jukumu la kulinda amani CONGO DRC.
No comments:
Post a Comment