Monday 18 May 2015

Majambazi Wakamatwa Wakitaka Kuiba Katika Benki ya NMB Tawi la Sinza Mori-Dar


Polisi jijini Dar wamewakamata watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi wakiwa katika jaribio la kuiba pesa katika benki ya NMB iliyopo Sinza-Mori, Dar.
 
Tukio hilo limetokea mchana wa leo katika Benki ya NMB tawi la Sinza-Mori jijini Dar ambapo majambazi hao walikamatwa wakiwa katika harakati za kutekeleza tukio hilo.
 
Majambazi hao baada ya kukamatwa wamepelekwa katika kituo cha Polisi Mabatini kilichopo Kijitonyama jijini Dar.

No comments: