
Mama mmoja amepatikana hai pamoja na mwanawe siku tano baada ya ndege walimokuwa wakisafiria kuanguka mwituni huko Colombia.
Mkuu wa jeshi la wanahewa la Colombian amesema tukio hilo ni la maajabu.''Kwa hakika hatujawahi kuona mtu ameishi baada ya ajali mbaya kama hii''alisema Kanali Hector Carrascal.

Bi Maria Nelly Murillo, 18, na mwanawe wa kiume mwenye umri wa mwaka mmoja walipatikana siku 5 baada ya ndege ya Cessna waliokuwa wakisafiria kuanguka katika msitu mkubwa ulioko katika jimbo la Choco.
Bi Murillo alikuwa na majeraha madogo huku mwanawe akionekana kuwa na afya nzuri.
Ndege hiyo yenye injini mbili ilikuwa ikisafiri kutoka Quibdo, hadi mji wa Nuqui iliyoko kwenye pwani ya Pacific kabla ya kuanguka siku ya jumamosi.
Hadi kufikia sasa haijulikani nini kilichosababisha ajali hiyo.
Hata hivyo milango ya ndege hiyo ilikuwa wazi na abiria waliokuwemo hawakuwepo.
Kundi la waokoaji lilianza shughuli ya kuwatafuta na baada ya siku tatu wakawapata bi Murillo na mwanawe.
Walipelekwa hospitalini kwa matibabu mjini Quibdo.
No comments:
Post a Comment