Hatimaye
vituo mbalimbali vya kuuza mafuta vimeanza kutoa huduma hiyo baada ya
kile kilichodaiwa ni mgoma baridi kumalizika huku bei mpya ikitawala
katika vituo vyote huku wananchi wakilalama juu ya bei hiyo mpya.
Tofauti na siku takribani tano zilizokuwa ni tete hasa kwa
watumiaji wa nishati ya mafuta kutokana na kile kinachodaiwa ni mgomo
baridi kwa makampuni makubwa ya mafuta kubana kutoa huduma hiyo kwa
kusubiri ujio wa bei mpya katika siku ya kwanza ya mwaka mpya wa
serikali, hatimaye bei mpya iliyowafanya vigogo hao wa uuzaji wa mafuta
nchini kubana nishati hiyo, sasa imewalazimu kuanza kutoa huduma hiyo
huku ikiwa na ongezeko kubwa la fedha jambo ambalo linatajwa kuwa
lianweza kuathiri shughuli za usafiri hasa kwa wananchi wa kipato cha
chini.
Wakati Tanzania ikitajwa kuwa miongoni mwa nchi zinazoendelea
ambapo pia zinakiwango kikubwa cha matumizi ya mafuta ya Petrol kwa siku
ambayo ni sawa na zaidi ya lita za ujazo milioni mbili na nusu kuanza
kwa bei hii mpya ya mafuta inatajwa kuwa na mafuaa kwa upande mmoja tu
wa shilingi.
No comments:
Post a Comment