Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro ACP Mussa Marambo amefika
katika eneo la tukio na kuthibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo
amesema chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa gari kutokuwa mwangalifu
wakati akivuka reli na nakuwataka madereva kuwa makini na kuzingatia
sheria wanapo vuka katika makutano ya reli na barabara ili kuepusha
ajali zisizokuwa za lazima zinazogharimu maisha ya watu.
Kwa upande wake mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Kilosa Dk
Denis Haule amekiri kupokea maiti 4 pamoja na majeruhi 25 ambapo kati
yao watano hali zao ni mbaya nawamehamishiwa katika hospitali ya rufaa
ya mkoa wa Morogoro kwa matibabu zaidi ambapo katika hatua nyingine
amelalamikia shirika la umeme Tanzania Tanesco kuweka umeme wa luku
katika hospitali ambapo wakatiwa tukio la ajali imesababisha kero kubwa
na kushindwa kuwahudumia majeruhi kwa wakati na kulazimika kuchukua muda
mrefu kutafuta jenereta.
Nao majeruhi na mashuhudia watukio hilo wameeleza jinsi tukio
lilivyotokea ambapo wametupia lawama dereva wa treni kutopiga honi kwa
tahadhari na kusababisha ajali ambayo imegharimu maisha ya watu kwa
kusabsiha vifo, na vilema vya kudumu kwa abira wasiokuwa nahatia.
Katika tukio hilo waliofariki ni mwanamke mmoja, wanaume wawili
pamoja mtoto mdogo na kati ya majeruhi 25 watano kati yao ni watoto
wadogo na wanaendlea na matibabu katika hospitali ya wilaya ya Kilosa
mkoani Morogoro
No comments:
Post a Comment