Maofisa wa afya nchini Sierra
Leone wametahadharisha uwezekano wa kutokea maambukizi zaidi ya virusi
vya ugonjwa wa Ebola ikiwa ni mwaka mmoja tangu mgonjwa wa kwanza
kubainika nchini humo. Wamesema kuwa hofu ya baadhi ya watu kukataliwa
na kutengwa na jamii ni moja ya sababu inayochangia kuenea kwa
maambukizi hayo kwani wengi hujificha wanapokumbwa na ugonjwa huo. Hata
hivyo kumekuwa na kasi ya kupungua kwa maambukizi ya ugonjwa huo katika
siku za hivi karibuni ,japo kuwa katika makao makuu ya nchi hiyo
Freetown hivi karibuni kumekuwa na maambukizi mapya ya ugonjwa huo.
Zaidi ya watu 4000 walikufa kutokana na ugonjwa wa Ebola nchini Liberia
na hivyo kuifanya nchi hiyo kuwa moja ya nchi tatu zilizoathirika na
Ebola,zikiwemo Guinea na Liberia.
No comments:
Post a Comment