Friday, 3 July 2015

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 03.07.2015.






JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
                                                 JESHI LA POLISI TANZANIA




 
RPC.                                                                                                  Ofisi ya Kamanda wa Polisi,                                                                                                                                                                                                                                                                                                  Mkoa wa Mbeya,                                                                                    
Namba ya simu 2502572                                                                                            S. L. P. 260,
Fax - +255252503734                                                                                                     MBEYA.
E-mail:-  rpc.mbeya@tpf.go.tz                                                                      
   tanpol.mbeya@gmail.com



TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 03.07.2015.




·         WATU WAWILI WA FAMILIA MOJA AUAWA KWA KUPIGWA FIMBO WILAYANI CHUNYA.




·         MWANAFUNZI WA DARASA LA TANO AFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA PIKIPIKI.





·         JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WAHAMIAJI HARAMU 13 RAIA WA NCHINI BURUNDI.




·         JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA KILOMBERO – MOROGORO AKIWA NA MILIPUKO [FATAKI] 78 BILA KIBALI.








KATIKA TUKIO LA KWANZA:

WATU WAWILI WA FAMILIA MOJA WALIOTAMBULIKA KWA MAJINA YA 1. YUNGE DOTTO (45) [MAMA ] NA 2. MAHONA ROBERT (16) [MTOTO] WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA TOTOE WALIUAWA KWA KUPIGWA FIMBO SEHEMU MBALIMBALI ZA MIILI YAO NA ROBERT MAKENZA (49) MKAZI WA KIJIJI CHA TOTOE [BABA] WA FAMILIA HIYO.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 01.07.2015 MAJIRA YA SAA 02:00 USIKU HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MWAWADIMI, KIJIJI CHA IYOVYO, KATA YA TOTOE, TARAFA YA SONGWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.

INADAIWA KUWA, CHANZO CHA TUKIO HILO NI MGOGORO WA KIFAMILIA BAADA YA MTUHUMIWA [BABA WA FAMILIA HIYO] KUITUHUMU FAMILIA YAKE KUMUOZESHA/KUMTOROSHA BINTI YAKE AITWAE KWANGU ROBERT (17) MKAZI WA TOTOE KWA MWANAUME KATIKA KIJIJI CHA MPONA.

AIDHA KATIKA TUKIO HILO, WATOTO WENGINE SITA WA FAMILIA HIYO WALIJERUHIWA NA WAMELAZWA KITUO CHA AFYA MBUYUNI KWA MATIBABU. MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO NA JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WANAFAMILIA KUTATUA MIGOGORO YAO YA KIFAMILIA KWA KUKAA MEZA MOJA YA MAZUNGUMZO ILI KUFIKIA MUHAFAKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.


KATIKA TUKIO LA PILI:

MWANAFUNZI WA DARASA LA TANO KATIKA SHULE YA MSINGI IDWELI ALITAMBULIKA KWA JINA LA TUMAIN EXAUD (16) ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.888 ABC AINA YA KINGLION ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA NZONGWA MBWILE (26) MKAZI WA IDWELI.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 02.07.2015 MAJIRA YA SAA 15:00 ALASIRI HUKO KATIKA KIJIJI CHA IDWELI, KATA YA ISONGOLE, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/TUKUYU.

CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI, MTUHUMIWA AMEKAMATWA NA UPELELEZI UNAENDELEA.








TAARIFA ZA MISAKO:

KATIKA MSAKO WA KWANZA, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA NDAHISHIMEYE JACRINE (34) MTUSI, MKAZI WA MAKAMBA – NYANZARI NCHINI BURUNDI NA WENZAKE 12 WAKIWEMO WATOTO WENYE UMRI KATI YA MIAKA 11/2 HADI MIAKA 15 WAPATAO 10 WOTE RAIA NA WAKAZI WA NCHINI BURUNDI WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI.

WAHAMIAJI HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 02.07.2015 MAJIRA YA SAA 17:30 JIONI HUKO VWAWA MJINI, KATA NA TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA.

INADAIWA KUWA, WAHAMIAJI HAO WALITOROKA KUTOKA KATIKA KAMBI YA ZEREKA – LILONGWE NCHINI MALAWI KWA MADAI YA HALI MBAYA YA HUDUMA HUSUSANI CHAKULA NA WALITOKA NCHINI KWAO BURUNDI MWAKA 2013 KUTOKANA NA MACHAFUKO. TARATIBU ZA KUWAKABIDHI IDARA YA UHAMIAJI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA ZINAENDELEA.



KATIKA MSAKO WA PILI:

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA KILOMBERO MKOANI MOROGORO ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ATSON MUBWA (50) BAADA YA KUKAMATWA AKIWA NA MILIPUKO [FATAKI] 78 ZILIZOTENGENEZWA KIENYEJI BILA KIBALI.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 01.07.2015 MAJIRA YA SAA 17:15 JIONI HUKO KATIKA STESHENI YA TRENI – TAZARA – IYUNGA, KATA NA TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA AKIWA KWENYE BEHEWA K2 NAMBA 3051 AKIWA NA TIKETI YA KUSAFIRIA YENYE NAMBA 00221 KUTOKA DSM – CTA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ZA MTU/WATU AU KIKUNDI CHA WATU ANACHOKITILIA MASHAKA KATIKA MAENEO YAO ILI UCHUNGUZI NA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.


Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments: