Rais
wa jamhuri wa Tanzania Mheshimiwa Dr,Jakaya Mrisho Kikwete amewaonya
baadhi ya viongozi wa dini nchini ambao wamekuwa na viashiria vya
itikadi za vyama vya siasa kuacha kuwabeba baadhi ya wagombea wa nafasi
mbali mbali za uongozi ikiwemo ya urais na wabunge kwa sababu inaweza
kusababisha choko choko za uvunjifu wa amani nchini.
Mheshiwa Rais Kikwete ametoa rai hiyo wakati wa sherehe za
maadhimisho ya Jubilee ya miaka 125 ya kanisa la kiinjili la kilutheri
nchini (KKKT) dayosisi ya kaskazini mashariki zilizofanyika katika
viwanja vya mbuyu kenda jijini Tanga na kuhudhuriwa na maelfu ya
wananchi, viongozi wa madhehebu ya dini pamoja na wageni kutoka taifa la
Ujerumani ambao ndio waanzilishi wa dhehebu hilo nchini.
Awali akizungumza na maelfu ya waumini wa madhehebu tofauti wa
ndani na nje ya nchi, askofu wa kanisa la kilutheri nchini dayosisi ya
kaskazini mashariki Dr Stephen Munga amemuomba mheshimiwa rais
kuhakikisha kuwa kipindi hiki cha uchaguzi mkuu ujao, nchi inaimarika
kwa kuwa na amani kwa sababu yeye ndiye mwenye mamlaka makubwa ya
kufikia malengo hayo kupitia chama chake.
Kufuatia hatua hiyo askofu mstaafu wa dayosisi ya kaskazini
mashariki Joseph Jali amekemea viongozi wanaowabeba baadhi ya wagombea
na kuonya kuwa rais hawezi kupatikana kwa njia ya nguvu zakibinadamu na
badala yake mwenyezi mungu ndiye anayejua kuwa Tanzania itaongozwa na
mtu atakayekuwa chaguo lake.
No comments:
Post a Comment