Sunday 5 July 2015

Dr Shein apitishwa kuwa mgombea urais wa Zanzibar kupitia CCM.


Kamati kuu maalum ya chama cha mapinduzi Zanzibar kwa kauli moja imempitisha Dr Ali Mohamed Shein kuwa mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama cha mapinduzi.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya wajumbe wa NEC wa Zanzibar wanounda kamati maalum ya Zanzibar kukutana hapa Zanzibar katika afisi kuu ya CCM na kuamua kumuidhinisha Dr Shein kugombea tena  kiti hicho cha urais baada ya wajumbe karibu 102  ambao ni aslimia 83  kuridhia Dr Shein agombee.
 
Awali Dr Shein ambaye ni makamu mwenyekiti wa CCM Zanzibar alilazimika kuondoka ndani ya kikao ili ijadaliwe na wanachama hao ambapo kiti hicho kilishikwa kwamuda na Dr Mohamed Gahribu Bilali makamu wa rais, ambapo baadaye akizumgumza na wanaccm hao waliokubali Dr Shein aliwahidi wanachama wa CCM kuwa  uamuzi wake uko palepale wa kutekeleza ilani ya CCM ya kuitumika Zanzibar.
 
katika hatua nyengine naibu katibu mkuu wa CCM Zanzibar akizungumza baada ya kikao hicho amesema CCM haiwezi kupinga au kukubali suala la majimbo wao wanasubiri maamuzi ya tume nawako tayari kwa umauzi wowote utakaotolewa natume ya uchaguzi ambayo inatarajiwa kutangaza majimbo mapya jumatatu asubui.
 
Kupitishwa kwa Dr Shein kugombea urais wa Zanzibar na kamati maalum ni hatua ya kwanza nasasa shuguli yote inahamia Dodoma ambapo jina la Dr Shein litajadiliwa na kamati kuu na baadaye kutakiwa kuidhinishwa na kupitishwa na halmashuri kuu ya CCM, nafasi ya urais wa Zanzibar inaamuliwa na NEC na siyo na mkutano mkuu waccm.

No comments: