Watanzania
wana haki ya kuwezeshwa tena kwa upendeleo maalum ili watumie fursa
zilizopo na uwepo wa utajiri wa raslimali za asili kujikwamua kiuchumi.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta binafsi nchini TPSF Dr Reginald
Mengi ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati Viongozi wa taifa na wa
mikoa wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania JWT walipokutana na
viongozi wa TPSF kujadili changamoto mbalimbali za biashara.
Amessma licha ya kuaminishwa kwa muda mrefu kuwa Tanzania ni nchi
maskini, lakini kama nchi Tanzania ina ujajiri mkubwa wa raslimali,
isipokuwa wananchi wake ndio maskini wanaohitaji serikali iwawezeshe ili
waweze kutumia fursa na raslimali hizo kujikwamua kiuchumi.
Wakati wa mkutano huo uliohudhuriwa pia na baadhi ya wanachama wa
JWT, waliazimia kuanzisha benki ya Wafanyabiashara baada ya kujiridhisha
kuwa benki zilizopo si rafiki kwao.
Aidha viongozi hao walijadili kwa kina kuhusu kuwaruhusu wachuuzi
wa kigeni kufanya biashara nchini zinazoweza kufanywa na watanzania, na
mpango wa serikali wa kutaka kuwapatia Wachina eneo la Kurasini ili
wajenge na kuendesha soko la kimataifa la bidhaa za viwandani, ambapo
wameitaka serikali isitishe mpango huo na kulikabidhi eneo hilo kwa
Watanzania ili kulinda biashara za Watanzania na uchumi wa Taifa.
Pia Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Bw. Godfrey Simbeye ameishauri
serikali kuuweka wazi mkataba wa kuliendeleza eneo hilo la biashara ili
ifahamike nafasi na ushiriki wa wafanyabiashara wa Tanzania, huku
Mwenyekiti wa taifa wa JWT Bw. Johnson Minja akisema mkutano huo ni
hatua muhimu kwa maslahi na maendeleo ya wafanyabiashara nchini.
Wanachama wa JWT walimzawadia Dr Mengi sampuli chache za bidhaa
wanazozitengeneza nje ha nchi kwa nembo zao binafsi za biashara na
kuziuza hapa nchini.
No comments:
Post a Comment