Wednesday 1 July 2015

WALIOMUUA ALBINO MWAKAJILA WA MBEYA WAHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA



Hakimu Mwakalinga siku alipohukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa mauaji ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe. Leo amehukumiwa tena kunyongwa mpaka kufa katika mauaji ya mlemavu wa ngozi Henry Mwakajila.
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Mbeya  imewahukumu kunyongwa mpaka kufa watu wanne kati ya watano waliomuua Henry Mwakajila (17) ambaye ni mlemavu wa ngozi (albino).
Waliohukumiwa kunyongwa mpaka kufa ni Asangalwisye Kayuni maarufu kama Katiti au Mwakatoga na Gerard Korosso Kalonge (wakazi wa Kijiji cha Mbembati wilayani Ileje), na Leonard Msalage Mwakisole na Hakimu Mselem Mwakalinga (wakazi wa Kiwira wilayani Rungwe).

Mshtakiwa wa nne, Mawazo Philemon Figomole, ameachiliwa huru na mahakama hiyo baada ya ushahidi wa upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha pasi na shaka kwamba alihusika katika mauaji hayo.
Akisoma hukumu ya kesi hiyo ya mauaji yenye kumbukumbu Namb. KIW/IR/49/2008 na PI 5/2013, Jaji wa Mahakama Kuu Dk. Revila, amesema mahakama imejiridhisha pasi na shaka na ushahidi wa upande wa mashtaka kwamba washtakiwa hao wanne walitenda kosa hilo na hivyo wanastahili adhabu hiyo.
Hii ni kesi ya saba ya mauaji ya albino kutolewa hukumu ambapo mpaka sasa jumla ya watuhumiwa 15 wamehukumiwa kunyongwa mpaka kufa. Ililezwa mahakamani hapo kwamba, mnamo Februari 5, 2008 majira ya saa 12:00 na saa 1:00 jioni huko katika Kijiji cha Ilolo, Kata ya Kiwira, tarafa ya Ukukwe, wilayani Rungwe katika Mkoa wa Mbeya, washtakiwa hao walimteka nyara kijana Henry Mwakajila, ambaye ni mlemavu wa ngozi aliyekuwa akisoma kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Ukukwe na kisha kumuua.
Wakati wa mwenendo wa kesi, ilielezwa na mashahidi wa upande wa mashtaka kwamba mshtakiwa wa kwanza Asangalwisye Kayuni maarufu kama Katiti au Mwakatoga ambaye ni mganga wa jadi, mkazi wa Kijiji cha Mbembati, Wilaya ya Ileje, alikutwa na utumbo unaodhaniwa kuwa wa binadamu na ulipopelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ukathibitika kwamba ni utumbo wa marehemu Henry

No comments: