Thursday 6 August 2015

Hapa Kuna Picha 7 Za Prof. Lipumba Akitangaza Maamuzi Magumu Ya Kujiuzulu Uenyekiti Wa CUF


Aliyekuwa  Mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kung'atua rasmi umwenyekiti wa chama hicho na kuendelea kuwa mwanachama wa kawaida wa chama hicho.
 
Lipumba  amesema ataendelea  kuwa mwanachama halali kwani kadi yake ya uanachama ameshailipia mpaka mwaka 2020.Ameyasema hayo katika ukumbi wa mikutano wa Peacock hoteli jijini Dar es Salaam leo.
 Aliyekuwa  Mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akiwa na wananchi wa kawaida kulia, Abdala Shabani  pamoja na mdogo wake,Shabaani Miraji wakiwa wamemsindikiza aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF taifa ili kuzungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya wananchi katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
 Waandishi wa habari wakimsikiliza Aliyekuwa  mwenyekiti wa chama cha CUFtaifa, Profesa Iblahimu Lipumba akitangaza  kujiuzulu wadhifa wake katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
Aliyekuwa  Mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akionyesha Rasimu ya Katiba pendekezwa ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kuwa ndio iliyosababisha kuungana na kuunda umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA)  katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
 Aliyekuwa  Mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akionyesha Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambayo katika mkutano wa kujivua uenyekiti wa chama cha CUF leo jijini Dar es Salaam.
Aliyekuwa  Mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akikusanya makabrasha yake mara baada ya kumaliza mkutano wa kujivua uenyekiti wa chama cha CUF taifa katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.

No comments: