Sunday 28 August 2016

Vurugu zatokea Mlowo Wilaya ya Mbozi baada ya  raia kufia mikononi mwa Jeshi la Polisi.





 

 

Wananchi wakimsikiliza Diwani wa Kata ya Mlowo Sebastian Kilindu akiwasihi kuwa na utulivu

Kamanda wa Polisi Mkoani Songwe akiongea na wananchi wa Mlowo ili kusuhisha mgogoro.

waombolezaji wakiwa nyumbani kwa dada wa marehemu eneo la Mlowo Mbozi Mkoani Songwe.

Hali ya uvunjifu wa amani umejitokeza Mji mdogo wa Mlowo Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe baada ya wananchi kuchoma moto barabarani kwa magurudumu ya magari barabara Kuu ya TANZAM Mbeya /Tunduma. Tukio hilo limetokea majira ya mchana Agost 28 mwaka huu baada ya wananchi wa Mlowo kudai kuwa mkazi mmoja aliyefahamika kwa jina la Stanslaus Kalinga (42)kupigwa na Askari baada kukamatwa kwa kosa la uzembe na uzururaji. Marehemu amefia hospitali ya Wilaya ya Mbozi akipatiwa matibabu.Diwani wa Kata ya Mlowo Sebastian Kilindu amekiri kutokea kwa tukio hilo na baadaye alikwenda Polisi ili kupata ukweli wa tukio hilo . Kamanda wa Polisi Mkoani Songwe Mathias Nyange amesema kuwa Jeshi la Polisi lilimkamata marehemu na hakupigwa na Polisi kama inavyodaiwa kwani taarifa kamili juu ya kifo hicho ataitoa baada ya uchunguzi wa Daktari. Katika hali isiyo ya kawaida wakazi wa Mlowo walibeba chakula kutoka msibani na kunipeleka kituo cha Polisi Mlowo kwa kile walichodai kifo cha marehemu kimesababishwa na Askari hivyo nao washiriki kula. Hali hiyo ilisababisha polisi kutumia mabovu ya machozi ili kuwatawanya  wananchi hao . Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mlowo alimuomba Kamanda wa Polisi Mkoani Songwe kufanya suluhu na wananchi hao kwa kuwa Askari hawana kambi wanaishi nao mitaani hivyo mgogoro huo utatuliwe kwa amani . Hata hivyo bado hali imekuwa tete kutokana na wananchi kughadhabika.

No comments: