Friday 7 July 2017

Jaji Mwingine Aomba Kustaafu Kabla ya Wakati.....Rais Magufuli Aridhia


SeeBait
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameridhia maombi ya kustaafu mapema kwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Prof. John Eudes Ruhangisa.

Taarifa iliyotolewa  na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Mhe. Rais Magufuli ameridhia maombi ya kustaafu mapema kwa Prof. John Eudes Ruhangisa kuanzia  06 Julai, 2017.

Mhe. Prof. John Eudes Ruhangisa alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya  Tanzania kanda ya Shinyanga.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

No comments: