Bweni
la wanafunzi katika shule ya sekondari Bunambiyu iliyopo katika kata ya
Bunambiyu wilayani Kishapu mkoa wa Shinyanga limeteketea kwa moto na
kuteketeza mali za wanafunzi 26 wa kike waliokuwa wanalala katika bweni
hilo.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Muliro Jumanne Muliro alisema tukio
hilo limetokea Julai 17,2017 majira ya saa mbili asubuhi.
Alisema
mwalimu wa shule hiyo Wilfred John (28) alibaini bweni kuungua moto na
kuteketeza mali za wanafunzi 26 wa kike waliokuwa wanalala katika bweni
hilo.
Kamanda
Muliro alisema chanzo cha moto bado hakijafahamika na kwamba thamani ya
mali zilizoteketea hazijafahamika na hakuna madhara kwa binadamu.
Wakati
huo huo,nyumba ya mfanyabiashara Amani Issa (39) mkazi wa kitongoji cha
Mhunze kata ya Mhunze wilayani Kishapu imeteketea kwa moto na
kusababisha hasara ya shilingi milioni 100.
Kamanda
Muliro alisema tukio limetokea Julai 17,2017 majira ya saa 10 jioni
katika kitongoji hicho cha Mhunze ambapo nyumba iliungua moto na
kuteketeza mali zilizokuwemo ndani zenye thamani ya shilingi
100,000,000/=.
Aliongeza kuwa hakuna mtu aliyedhurika na chanzo cha tukio kinachunguzwa.
No comments:
Post a Comment