Friday 14 July 2017

Mfumo mpya huu utawaondoa watumishi waliostaafu kila ifakapo saa sita usiku



“Kuna watumishi ambao muda wao wa kuwepo kazini umemalizika (wamestaafu) lakini bado wanaendelea kuwepo, mfumo wa HCMIS sasa kila ifikapo saa 06:01 usiku utakuwa unawaondoa wale wote ambao muda wao wa kuwepo kazini umefika, lakini bado wanaendelea kuwepo kwenye Mfumo,” amesema.

Kairuki amesema uhakiki wa kina utasaidia kuepuka kutojirudia tena kwa suala la watumishi wa umma wanaoghushi vyeti.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, amesema hayo leo Alhamisi, Julai 13 katika kikao kazi na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Amewataka wWaajiri kusafisha taarifa za watumishi wa umma mara kwa mara katika Mfumo Shirikishi wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS).

No comments: