Baada
ya mkazi wa Mharani kwa Matiasi wilayani Kibaha kukutwa amefariki dunia
kwa kuuawa na watu wasiojulikana jana majira ya saa moja usiku, Kamanda
wa Polisi mkoani Pwani Jonathan Shana ametangaza mapambano makali ya
kuwatia nguvuni wahalifu.
Kamanda
Shana amesema kuwa mwili wa mwanamke huyo aliyetambuliwa kwa jina la
Mariamu Omari (31) ulikutwa nje ya nyumba anayoishi mbele kidogo umbali
wa mita 40 akiwa anavuja damu nyingi sehemu za usoni na jereha kichwani
upande wa kushoto huku muuaji akiwa bado hajafahamika.
No comments:
Post a Comment