WAZIRI
wa afya, jinsia, wazee na watoto, Ummy Mwalimu amemsimamisha kazi
mganga mfawidhi wa kituo cha afya Mlandizi, Dk. Mpola Tamambele,
kutokana na kushindwa kusimamia maelekezo ya serikali ya kuhakikisha
mama mjamzito, mtoto chini ya miaka mitano na mzee wanapata huduma bure.
Kutokana
na kutokuwa na mamlaka ya moja kwa moja amemuagiza Kaimu Mkurugenzi wa
halmashauri ya halmashauri ya wilaya ya Kibaha, Beda Mmbaga kumsimamisha
kazi mganga mfawidhi huyo mara moja wakati uchunguzi wa tuhuma
zinazomkabili zikiendelea .
Amemuelekeza
Kaimu Mkurugenzi huyo pia kuwafuatilia watumishi wa afya kituoni hapo
waliohusika kumuagiza mama aliyejifungua Salma Khalifan kwenda kununua
vifaa vya kujifungulia vya sh.180,000 ili apate huduma .
Aliyasema
hayo wakati alipokwenda kutembelea kituo cha afya Mlandizi, kabla ya
kukabidhiwa kwa magari ya wagonjwa matatu kutoka kwa mbunge wa jimbo
hilo, Hamoud Jumaa.
Waziri
huyo alisema yeye hana mamlaka ya moja kwa moja kumsimamisha kazi
mganga mfawidhi huyo hivyo anaiachia mamlaka husika isimamie jukumu
hilo. Alisema hatokubali kuona watumishi wachache kwenye vituo vya afya,
zahanati na hospitali wanachezea maagizo ya serikali. Alifikia hatua
hiyo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa mama aliyejifungua ambae
alisema amenunua vifaa vya kufanyiwa operesheni kwa gharama ya sh .180,
000.
Ummy
alisema haiwezekani kuona mama wajawazito, wanalipishwa hadi gloves na
pamba ili kujifungua wakati serikali yao ilishasema watahudumiwa bure .
Alieleza kwamba, kuanzia sasa waganga wakuu wa wilaya, mikoa na
watumishi wa afya wote nchini wahakikishe wanatimiza maelekezo ya
serikali kuhudumia akinamama wajawazito na watoto ili kupunguza vifo vya
uzazi . Ummy alisema kuwa ,watumishi na wauguzi wengi wanajituma na
kufanya kazi zao kifanisi ila wapo wachache ambao wanakwamisha juhudi
hizo .
"Sitokubali
mtumishi anakwenda kinyume na serikali ,rais wetu John Magufuli
anasisimamia suala zima la kuboresha huduma za afya ,halafu akitokea mtu
mmoja mzembe anatuchanganya kwakweli sitoweza kumfumbia macho "
"Wananchi
wamekuwa waoga hata kuingia katika suala la bima ya afya kwa sababu ya
mambo kama haya ,namsimamisha mganga mfawidhi huyo hadi hapo uchunguzi
utakapokamilika ." alisema Ummy .
Mbali
ya hayo Ummy alibainisha,bajeti ya dawa katika halmashauri ya wilaya
ya Kibaha imeongezeka ndani ya miaka miwili mfululizo kwenye uongozi wa
serikali ya awamu ya tano .
Waziri
wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akitembelea kituo cha
afya Mlandizi katika ziara yake aliyoifanya jana. kushoto ni Mganga
Mfawidhi wa kituo cha afya Mlandizi, Dk. Mpola Tamambele, ambaye
amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi.
Ummy
alisema mwaka 2015/2016 bajeti ya madawa katika halmashauri hiyo
ilikuwa mil.24 na 2017 ilifikia mil.70 na bajeti ya sasa 2017/2018
imefikia sh. mil.101 .
Kwa
upande wake mama aliyejifungua kituoni hapo ,Salma Khalfani ,alimweleza
Ummy kwamba aliandikiwa orodha ya dawa za kununua kwenye maduka ya dawa
ya nje .
Alieleza
,alitakiwa kufanyiwa upasuaji na hivyo kutakiwa kununua madawa na
vifaaa tiba ,pamba na gloves vya 180,000 akanunue ili aweze kujifungua .
Kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo ,Mmbaga alisema maagizo aliyopewa na waziri ameyapokea na atayafanyia kazi .
Nae
mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini, Hamoud Jumaaa alisema kumekuwa na
malalamiko mengi juu ya wananchi hasa akinamama kulipishwa fedha za dawa
na vifaa tiba. Alisema baadhi ya wazee wamekuwa wakishindwa kupewa
huduma za afya bila malipo. Jumaa alimuomba Ummy kuendelea kushirikiana
nae kuwadhibiti watumishi wazembe wanaodidimiza haki za wananchi .
No comments:
Post a Comment