Mahakama
Kuu ya Tanzania imewahukumu askari Polisi wawili wa kutoka kituo cha
Oysterbay jijini Dar es Salaam na watu wengine sita kwenda jela miaka 35
kwa makosa mawili ya kukutwa nyara za serikali na kujihusisha na
mtandao wa ujangili.
Hayo
yamesemwa na Wakili wa Serikali, Salimu Msemo alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari mjini Dodoma, ambapo aliwataja polisi hao wa zamani
waliokutwa na hatia ni wenye namba D 8656 CPL Senga Nyembo na G 553 PC
Issa Mtama washtakiwa walikutwa na meno 70 ya tembo yenye thamani ya Sh.
milioni 800.
Wengine
sita waliokuwa nao wote wamekutwa na hatia ni pamoja na Prosper Maleto,
Seif Mdumuka, Amri Bakari, Said Mdumuka, Ramadhan Athuman na Musa
Mohamed.
Aidha,
amesema kuwa washtakiwa hao walikutwa na kosa hilo katika eneo la kituo
cha ukaguzi cha Kauzeni lililopo Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani kabla
ya kufikishwa kortini na kukumbana na adhabu hiyo.
Hata
hivyo, ameongeza kuwa katika kosa la kwanza, washtakiwa walihukumiwa
kwenda jela miaka 20 kila mmoja na faini kwa kila mmoja, wakati katika
kosa la pili, washtakiwa wawili ambao ni hao polisi, walihukumiwa miaka
15 kwenda jela.
No comments:
Post a Comment