Mwanamke aliyejulikana kwa jina la Zena
Mohamed (28) msukuma amemuua mme wake Bakari Salehe (35) Mzaramo kwa
kumchinja na kisu shingoni upande wa kushoto.
Tukio hilo limetokea jana saa mbili na nusu usiku Septemba 20,2017
katika kitongoji cha Malenge kijiji cha Jomu,kata ya Tinde,tarafa ya
Itwangi,wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga.
Inaelezwa kuwa wanandoa hao walikuwa wamegombana,ndipo mke akamsubiri
mmewe alale na alipolala akamchoma kisu tumboni na shingoni.
“Baada ya kutekeleza tukio hilo,mwanamke huyo alifungua radio kwa
sauti ya juu kisha kumfunga mlango kwa kufuli kisha kukimbilia Shinyanga
Mjini ambapo kuna Mama yake mzazi,alipofika akamwambia mama kuwa
amefanya mauaji,hali iliyomfanya mama atoe taarifa polisi na kufanikisha
kukamatwa kwa mtuhumiwa”,mashuhuda wamesema
Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Haule amesema
tukio hilo limetokea wakati wanandoa hao walipokuwa wanapigana katika
ugomvi uliotokea nyumbani kwao.
“Chanzo cha tukio hilo ni wivu wa mapenzi baada ya mke kupokea simu
ya mume wake iliyokuwa ikiita na kisha kusikia sauti ya mwanamke
mwingine na kuhisi kuwa ni hawala wa muwe wake,ndipo ugomvi
ulipoanzia”,ameeleza Kamanda Haule.
Kamanda huyo wa polisi amesema wanamshikilia mtuhumiwa kwa mahojiano
zaidi na ametoa wito kwa wananchi kujiepusha na kuachana na vitendo vya
dhana ya wivu wa kufikirika.
“Tuache kufikiri kuwa mwanaume akiongea na mwanamke au mwanamke
akiongea na mwanaume kwa njia ya simu au njia ya kawaida lazima kuna
mahusiano ya kimapenzi,jambo ambalo siyo kweli hasa kutokana na masuala
ya utandawazi katika dunia hii ya leo”,ameeleza Kamanda Haule.
No comments:
Post a Comment