Monday, 25 September 2017

Rais Magufuli Kuongoza Vikao vya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa - NEC Kwa Siku Mbili Dar


SeeBait
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Taifa, anatarajia kuongoza kikao cha  Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kwa siku mbili Jijini Dar es Salaam, Septemba 30 hadi Oktoba 1, 2017.

Kwa mujibu wa  taarifa iliyotolewa jana  Septemba 24 na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole ameeleza kuwa, Kamati kuu ya Halmashauri ya Taifa (CC)  na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) vinatarajia kuketi  Jijini Dar e Salaam kwa nyakati tofauti.

No comments: