Mara
baada ya kikao cha kwanza kwenye mkutano wa 8, wa Bunge la 11, Spika wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai amesema wale
waliokuwa wanamtuhumu kuwa mdhaifu katika kufanya maamuzi, sasa wataona
dhahiri udhaifu wake uko wapi.
Spika
Ndugai ameeleza hayo wakati akiwakaribisha wabunge 7 wapya wa Chama cha
Wananchi (CUF) waliotangazwa na Tume ya Uchaguzi kuchukua nafasi ya
wabunge nane ambao walivuliwa uanachama na kupoteza sifa ya kuwa wabunge
na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba.
“Taratibu
zote zilifuatwa kwa wabunge hawa kuingia hapa bungeni, wapo baadhi ya
lile kundi wiki mbili kabla ya mambo haya kutokea walisema Spika dhaifu,
nikasema sasa udhaifu wangu ndiyo utaonekana. Kama una akili yako
maneno kama haya hayana umuhimu”, alisema Spika Ndugai.
Sambamba
na hilo, Spika Ndugai amewakaribisha wabunge walioapishwa huku
akiwafunda wabunge wengine, kwamba kiapo walichokula wenzao leo
kiwakumbushe utii na uaminifu kwa kwa tiba ya nchi.
“Kiapo
hiki cha uaminifu kina tukumbusha wengine ambao tuliapa utii wa Katiba
na kiapo chetu kwa ujumla wake, kuhusiana na uaminifu na utii. Ni
vizuri kuisoma Katiba na kuipitia ili uweze kujua nafasi ya vyama vya
siasa na uhusiano wa mbunge na chama cha siasa”, alisisitiza Spika
Ndugai.
Wabunge
hao ambao wameapishwa leo wanatarajiwa kupangiwa kamati na kuanza kazi
mara moja, kama ambavyo Spika amewataka kufanya hivyo.
No comments:
Post a Comment