Maafisa
92 wa polisi nchini Kenya wamelazwa hospitalini Nairobi na viunga vyake
wakihofiwa kuugua ugonjwa wa kipindupindu, wizara ya afya nchini humo
imesema.
Maafisa
hao wamelazwa katika hospitali ya taifa ya Kenyatta, hospitali ya Sinai
na katika hospitali ya wanawake ya Nairobi Women’s.
“Polisi
hao inashukiwa waliambukizwa kipindupindu katika mgahawa wa polisi
katika eneo la Nairobi Area,” taarifa ya wizara hiyo imesema.
Mgahawa huo umefungwa kwa muda usiojulikana huku uchunguzi ukiendelea.
Waziri Cleophas Mailu amesema maafisa hao wanaendelea kupata nafuu hospitalini.
Gazeti
la kibinafsi la the Star linaweza baadhi ya maafisa walikuwa kazini
wakati wa kutangazwa kwa uamuzi wa mahakama kuhusu kesi ya kupinga
matokeo ya uchaguzi wa urais.
Gavana wa Nairobi Mike Sonke alikuwa Jumapili ametoa taarifa na kusema hali imethibitiwa.
Alisema hatua zimechukuliwa “kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo.”
No comments:
Post a Comment