Muda
mfupi baada ya kiongozi wa upinzani Kenya Raila Odinga kutangaza
kutoshiriki katika marudio ya Uchaguzi Mkuu mpaka Tume ya Uchaguzi
ifanyiwe mabadiliko, Tume hiyo imetangaza kundi la watu sita ambalo
litasimamia uchaguzi huo.
Walioteuliwa
ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo Ezra Chiloba, Naibu wake Betty Nyabuto,
Mkurugenzi wa Usajili wa wapiga kura pamoja na Mkuu wa Operesheni za
Uchaguzi Immaculate Kasait, Naibu wake Mwaura Kamwati, Mkuu wa
Operesheni za Tume na Mkuu wa Teknolojia James Muhati.
Uchaguzi
wa marudio Kenya umepangwa kufanyika October 17, 2017 kutokana na
ruhusa ya Mahakama ya Juu nchini humo kufuatia kesi ya kupinga matokeo
iliyofunguliwa na Odinga.
No comments:
Post a Comment