Serikali
imekanusha vikali taarifa kutoka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
kuwa ina mahusiano ya kibiashara na Korea Kaskazini ambayo imewekewa
vikwazo vya kiuchumi na baraza hilo.
Hayo
yamesemwa jana jijini Dar es salaam na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga, alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari, ambapo alisema kuwa licha ya
uhusiano uliokuwepo awali, lakini tangu mwaka 2014, Tanzania imepunguza
uhusiano wa kibiashara na kidiplomasia na nchi hiyo.
“Hatuna
ugomvi na Korea Kaskazini, lakini kwa mpango wake wa kutengeneza
makombora ya masafa marefu ya nyuklia sio mzuri kwa heshima na usalama
wa duniani, ndiyo maana tukaanza kuchukua hatua za kupunguza mahusiano.” alisema Dkt.Mahiga
Aidha,
Dkt. Mahiga aliongeza kuwa uhusiano huo wa kibiashara ulikuwepo kabla
ya vikwazo vilivyowekwa hivi karibuni na Baraza la Umoja wa Mataifa
Tanzania
na Uganda ni miongoni mwa baadhi ya nchi zinazochunguzwa na Umoja wa
Mataifa kwa tuhuma za kwenda kinyume na vikwazo vilivyowekwa na Baraza
la Usalama la Umoja wa Mataifa dhidi ya Korea Kaskazini.
Ripoti
ya uchunguzi huo ilitolewa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa tarehe
9 mwezi wa Septemba. Baraza la Usalama la Umoja ikisema linachunguza
tuhuma za Tanzania kuingia mikataba ya kijeshi na Korea Kaskazini
inayogharimu dola za kimarekani milioni 12.5
No comments:
Post a Comment