Sakata
la upungufu wa nguvu za kiume ambalo limekuwa changamoto kubwa kwa
baadhi ya wanaume miaka ya sasa, limeibua sintofahamu bungeni baada ya
mbunge wa Konde, Khatibu Saidi Haji (CUF) kutaka kujua serikali
imejipanga vipi katika kukabiliana nalo.
Akijibu
swali hilo Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Hamisi Kigwangala amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kusema
serikali haina jibu la moja kwa moja kuweza kuwapa wananchi, kwani tendo
la ndoa hufanyika faragha baina ya wanandoa.
Dkt.
Kigwangala aliendelea kusema kwamba pamoja na usiri uliopo kuhusu
tatizo hilo, lakini kuna vitu wanaweza kufanya ili kukabiliana nalo,
ambapo huweza likasaidia kuokoa ndoa yao na kuweza kuwapatia watoto.
"Nianze
kukubaliana na Mhe. Hatibu Said Haji kwa swali la msingi, changamoto za
ukosefu wa nguvu za kiume zinazowapata wanaume wengi sasa hivi,
zinatokana na ukosefu wa furaha, msongamano wa mawazo na ongezeko la
magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama kisukari, shinikizo la damu, ukiwa na
matatizo haya huwezi kuwa na furaha katika tendo la ndoa", alisema Dkt. Kigwangala.
Naibu
huyo wa Wizara inayohusika na masuala ya Afya aliendelea kwa kuwataka
wananchi watafute furaha binafsi ili kuweza kuwa na hamasa ya kufanya
jambo hilo, na kuacha kuamini kwenye dawa za asili ambazo zimekuwa
zikiuzwa kiholela bila kuzingatia usalama wake kwa afya ya mtumiaji
No comments:
Post a Comment