Msanii Aslay ambaye sasa hivi anafanya
vizuri zaidi huku akiachia kazi mpya kila siku, amewataa mashabiki
kutompambanisha na Alikiba au msanii yeyote, kwani hajaweza kufikia
nafasi ya Alikiba.

"Sio kitu kizuri upande wangu, kwa sababu Alikiba kazi yake inaonekana na anafanya vizuri, kwa hiyo ukisema unanipambanisha mimi na Alikiba itakuwa sio picha nzuri, na sio Alikiba tu, msanii yeyote msinipambanishe naye, ambaye tayari yupo level zingine ", amesema Aslay.
Aslay ambaye anaendelea kutrend namba moja siku ya nne mfululizo, amesema kwenye sanaa kila mtu na uwezo wake, na iwapo atajiona ni top kwenye game atakuwa anakosea kwa sasa ila anatamani siku moja kuwa namba moja na kuwa msanii mkubwa zaidi na kufika mbali zaidi.
No comments:
Post a Comment