Rais Uhuru Kenyatta amemjia juu Kiongozi
wa NASA Raila Odinga baada ya kutangaza kutoshiriki uchaguzi wa marudio
ambao unatarajiwa kufanyika Oktoba 26 mwaka huu nchini Kenya na kusema
hata kama amejitoa Katiba ya Kenya haijazuia uchaguzi kutofanyika
Kenyatta amesema kuwa Odinga alitaka uchaguzi urudiwe jambo ambalo
limeigharimu nchi ya Kenya fedha nyingi ambazo zingeweza kutumika
kujenga barabara, zingeweza kutumika kujenga mahospitali na kutoa huduma
mbalimbali kwa wananchi, lakini anashangaa mtu ambaye ametaka uchaguzi
kurudiwa anajiengua tena.
"Rafiki yangu nasikia sasa umesema umejitoa baada ya kutupeleka peleka
zaidi ya shilingi bilioni 12 hivi sasa zinatumika ili tufanye uchaguzi,
pesa ambazo zingeweza kutumika kujenga barabara, zingetumika kujenga
hospitali ya wananchi sasa zinatumika kwa uchaguzi ambao yeye ndiye
aliitisha na sasa anasema hataki, kuna haki hapa jamanii, si mahakama
ilisema IEBC haina makosa hayo masharti yote unatoa lakini tume hii si
ndiyo imefanya viongozi hawa wengine wote kupatikana" alihoji Kenyatta
Mbali na hilo Kenyatta amesema kuwa wao wataendelea na mchakato wa
uchaguzi kama kawaida na kusema huenda awepo au asiwepo Odinga uchaguzi
utafanyika kama kawaida kama ambavyo tume ya uchaguzi ilitangaza.
No comments:
Post a Comment