Mwanaume aitwaye Joseph Sahani (60) mkazi wa kijiji cha Nzonza kata ya Salawe tarafa ya Nindo wilaya ya Shinyanga
amefariki dunia akiongezewa nguvu za kiume kwa
mganga wa kienyeji Robert Nkoma (58) kwa kujazwa dawa kwenye tundu la uume kwa kutumia pampu ya
baiskeli.
Kamanda wa Jeshi la polisi
mkoa wa Shinyanga Simoni Haule amesema tukio hilo limetokea jana majira ya saa 10 jioni.
"Chanzo cha tukio ni kwamba marehemu alikuwa na tatizo
la upungufu wa nguvu za kiume na kuamua kwenda kwa mganga huyo ili atibiwe ndipo
mganga akatumia njia ya kumuingiza unga unaosadikiwa kuwa ni dawa ya kienyeji
kwenye tundu la uume kwa kutumia pampu ya baiskeli akawa anapampu kama anajaza upepo na
kusababisha marehemu kuishiwa nguvu na kutoka damu nyingi kwenye uume na
kusababisha kifo chake”,ameeleza Kamanda Haule.
Tayari mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi la polisi.
No comments:
Post a Comment