Mkuu
wa Wilaya ya Tarime Mhe. Grolius Luoga akizungumza na watoto wakati wa
kongamano la kuzuia mimba za utotoni kuelekea kilele cha Maadhimisho ya
Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike yanayofanyika tarehe 11 Oktoba 2017
katika wilaya ya Tarime mkoani Mara.
Mkurugenzi
wa Maendeleo ya Watoto Bi. Magreth Mussai akiwasalimia watoto
waliojumuika kwenye kongamano la kuwajengea watoto uelewa wa kujilinda
dhidi ya ndoa za utotoni siku moja kabla ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto
wa Kike Kitaifa yanayofanyika tarehe 11 Oktoba, 2017 wilaya ya Tarime
mkoani Mara.
Mwakilishi
wa watoto wilayani Tarime Anna Simon akiwakilisha watoto wa wilaya ya
Tarime kutoa salamu za watoto kwa Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Tarime Bw.
Glorius Luoga(hayupo pichani) wakati wa mjadala wa ulinzi wa watoto
katika ngazi ya familia, shuleni, mtaani na jamii kwa ujumla.
Baadhi
ya watoto, wazazi, walezi na wazee wa mila katika wilaya ya Tarime
wakifuatilia kwa makini nasaha za Mkuu wa Wilaya ya Tarime Mhe. Grolius
Luoga(hayupo pichani) kuhusu wajibu wa kuwalinda watoto dhidi ya mimba
za utotoni katika wilaya ya Tarime, mkoani Mara.
Mkuu
wa Wilaya ya Tarime Mhe. Grolius Luoga akipokea zawadi ya vitabu kutoka
kwa mwakilishi wa watoto Anna Simon mara baada ya kufungua kongamano la
watoto wilaya ya Tarime, mkaoni Mara.
Mkuu
wa Wilaya ya Tarime Mhe. Grolius Luoga akiwa katika picha ya pamoja na
wadau wa ulinzi na usalama wa mtoto katika ngazi ya jamii wilaya ya
Tarime, mkoani Maramara baada ya kufungua kongamano la watoto.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
No comments:
Post a Comment