Rais wa Catalonia Carles Pugdemont
Rais wa Catalonia Carles Pugdemont ,
amesaini hati ya kuwa huru,lakini ametoa muda zaidi wa mazungumzo na
serikali ya Hispania kuhusiana na kujitenga kwao.
Haijafahamika mara moja kama hati hiyo
iliyosainiwa inakubalika kisheria,kwa kuwa kura ya maoni iliyopigwa siku
tisa zilizopita ilikuwa kwa mjibu wa mahakama ya katiba.
Hata hivyo kujitenga kwa jimbo la Catalonia kutatakiwa kusubiria idhini ya bunge la Catalonia.
Puigdemont awali aliliambia bunge kuwa
jimbo hilo limeshinda kuwa na haki ya kujipatia uhuru wake kama
taifa,Lakini serikali ya Hispania imeahidi kuzuia namna yoyote ya
kujitenga kwa jimbo hilo.
Chanzo:BBC
No comments:
Post a Comment