Na Agness Francis, Blogu ya jamii.
Baraza
la Sanaa Taifa(BASATA) limemfungia rasmi mmiliki wa Click Media
Entertainment, Edward Majura kujihusisha kuendesha matukio yeyote ya
sanaa hasa la utendaji wa mashindano ya urembo hapa nchini kwa muda
usiojulikana.
Akizungumza
hayo katibu mtendaji (BASATA) Godfrey Mngereza katika ofisi za (BASATA)
jijini Dar es Salaam amesema kuwa Edward Majura ambaye ni mtendaji wa
mashindano ya urembo miss Mbeya amekiuka sheria, kanuni na taratibu za
uendeshaji wa mashindano hayo hapa nchini .
Vilevile
katibu Mngereza amewataka wadau na waandaaji wote wa matukio ya sanaa
kuhakikisha wanafuata taratibu zote zilizowekwa ikiwa ni pamoja na
kupata vibali na kufanya kazi kwa karibu na ofisi za utamaduni katika
ngazi za wilaya na kimkoa pindi wanapohitaji kufanya tukio lolote la
sanaa na hapa nchini.
Aidha
Katibu mtendaji huyo ametanabaisha kuwa muandaaji yoyote atakae tumia
wakala walioko nchini katika tukio lake la sanaa atawajibika kuhakikisha
wako chini yake na wanafata sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji wa
tukio husika, ambapo kinyume na makubaliano hayo ( BASATA) haitasita
kumchukulia hatua yoyote ya kisheria.
Hata
hivyo Mngereza ametoa tamko kuwa wadau wote nchini watakaoendesha
matukio yoyote ya sanaa ikiwemo mashindano ya urembo wanatakiwa
kuwasilisha zawadi zao sehemu husika ambayo ni (BASATA) katika ofisi za
utamaduni siku 14 kabla ya kilele cha mashindano hayo.
Katibu
mtendaji (BASATA) Godfrey Mngereza akizungumza na waandishi wa habari
pamoja na wadau wa sanaa nchini kuhusu kufata kanuni na taratibu za
kufanya matukio ya sanaa hasa na mashindano ya urembo katika ofisi za
BASATA jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment