Friday 13 October 2017

USAJILI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA

Mwenyekiti wa mtaa wa akimsaidia kujaza fomu ya kitambulisho cha Taifa mmoja wa wananchi waliojitokeza kusajiliwa katika zoezi la usajili wa Vitambulisho vya Taifa wilayani Kyela mkoani Mbeya.
Usajili Vitambulisho vya Taifa Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya umeanza katika Kata za Matema, Makwale, Mababu na Ndobo na unatarajiwa kumalizika Jumamosi Octoba 14, 2017 na kuendelea Kata zingine.

Kwa mujibu wa msimamzi wa zoezi hilo Kanda ya Mbeya ndugu Magohu Zonzo amesema mwitiko mkubwa wa wananchi unatoa imani ya zoezi hilo kumalizika ndani ya siku zilizopangwa na kutoa fursa kwa Kata zingine kusajiliwa.  

Ameeleza faida za Mfumo wa Utambuzi na Usajili wa watu kwa Taifa na namna kila mwananchi atakavyonufaika na mfumo huo utakapoanza kutumika na hivyo kutoa wito kwa jamii hususani wananchi wa Wilaya ya Kyela kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kusajiliwa.

Zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa limeanza kwa kishindo mikoa ya Kanda ya Ziwa na Kaskazini na linakusudiwa kumalizika ndani ya muda mfupi kutoa fursa kwa mikao mingine ya Tanzania kusajiliwa.
 Mmoja wa wakaazi wa Mbeya akiweka saini ya kielektroniki wakati wa zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa linaloendelea wilayani Kyela.
 Baadhi ya wananchi wakisubiri kusajiliwa wakati wa zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa wilayani Kyela, wakati wengine wakiendelea Kusajiliwa na Maafisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa wakati zoezi linaendelea.
 Wakazi wa kijiji cha Kisyosyo Kata ya Matema wilayani Kyela mkoa wa Mbeya wakichukuliwa alama za vidole wakati wa zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa katika mkoa wa Mbeya.
Labels:

No comments: