Diwani
wa kata ya Sombetini Arusha Ally Bananga (CHADEMA) amewataka madiwani
waliopo ndani ya chama chao wanaotaka kuhama ndani ya chama waondoke
mapema kwani wakija kuwagundua kipindi cha uchaguzi kwamba ni wasaliti
watawatawanya viungo.
Bananga
amelazimika kutoa kauli hiyo baada ya wimbi la madiwani Arusha kuhama
chama hicho kwa tuhuma za kupokea rushwa, ambapo ameweka wazi kwamba
anaamini kwamba hakuna tatizo la madiwani kuhama vyama kwani ni uhuru
kama ilivyo kwa mashabiki wa simba kwenda Yanga kwa ajili ya maslahi yao
lakini wasiondoke kwa kununuliwa kwani haitakuwa busara na mwisho wa
siku itakuwa ni matatizo.
"Sina
tatizo kwa madiwani kuhama hata kidogo. Lakini kama ni kuhama kwa
kununuliwa kama hivi tunavyoona hili ni tatizo. Kama huna imani ondoka
mapema kwa amani. Tupishe kwa sababu tunaelekea kwenye uchaguzi na
tunaamini tutashinda kata zote, sasa isije ikatokea mbeleleni
tukakugundua kwamba wewe ni msaliti maana tutatawanyana viungo kitu
ambacho siyo kizuri. Ondokeni kwa amani yote sasa hivi mapema" -
Bananga.
Aidha
Bananga amesema kwamba amesikia maneno yaliyozungumzwa na aliyekuwa
Diwani wa Kimandolu, Mchungaji Rayson Ngowi na kueleza kwamba hawezi
kumsemea neno baya kwani ni rafiki yake lakini pia amemtaka asifanye
madhabahu ya Mungu kama kaunta ya 'bar' kwani ni mtu anayemfahamu na
wanajuana ni mangapi wamefanya pamoja hivyo asijisahaulishe.
"Namheshimu
sana Ngowi. Lakini amekubali kufika bei mimi nilishajua siku nyingi na
nilimwambia. Hata watu waliokuwa wakiongea naye waliniambia. Ametafuta
laana ya Mungu, yeye anajiita Mchungaji jambo ambalo nina wasiwasi nalo.
Lakini kwa maneno aliyoyasema kwenye mkutano Soko kuu lakini ndiyo
ameshanunuliwa, Mungu siyo mjomba yake na Madhabahu asiigeuze kama
kaunta." Bananga ameongeza
Ameongeza
kwamba "Adhabu ya Mungu inamfuata kabla ya adhabu yetu sisi Chadema
tutakayompatia wakati atakapogombea. Kama yeye ni mwanaume asogeze pua
yake kwenye uchaguzi huu mdogo aone tutakavyomfanya".
Pamoja
na hayo Bananga amesema anaamini ushindi katika uchaguzi mdogo lazima
watashinda kwani wamekuwa bora chini ya uongozi wa Mbunge Godbless Lema
na Meya Calist Lazaro na kutokana na ushahidi wa Nassari kuonyesha
wabunge walikuwa wakinunuliwa kama maandazi safari wamejiandaa kupeleka
keki kwenye chaguzi.
No comments:
Post a Comment