|
Meli ya kivita ya kupambana na uharamia
aina
ya Anti Submarine iitwayo Marshal Shaposhnikov’, ilipokuwa ikiingia
na kasha baadae kutia nanga katika bandari ya Dar es Salaam, kwa ziara
fupi yenye lengo la kuimarisha urafiki baina ya Jeshi la Wanamaji wa
Tanzania na Urusi. Wakati nchi ya Somalia ikiendelea kuwa kitovu
cha uharamia, jumuiya ya kimataifa ilikubaliana kudhamiria kupambana na
vitendo hivyo viovu. Lakini hadi sasa, wakati nchi nyingine zikitumia
mbinu mbalimbali katika mapambano hayo, ni nchi za Russia, India na
China pekee zinazosindikiza meli zao za biashara na nyinginezo ili
kuzilinda na uharamia. Meli hiyo imewasilisiku ya Jumamosi na inategemea
kuondoka kesho, Jumatano.
|
|
Balozi wa Urusi hapa nchini Mheshimiwa Alexander Rannikh akiambatana
na kiongozi wa wanajeshi waliofatana na meli hiyo Rear Admiral Vdovenko |
|
Kwa pamoja, Balozi Rannikh na
wanajeshi
wa Kirusi waliimba wimbo wao wataifa wakiwa katika meli.
|
|
Balozi
Rannikh akiwapongeza wanajeshi wake kwa kufika Dar es Salaam, Tanzania
na kuwakaribisha nchini pia. |
|
Baada
ya salamu hizo, Balozi Rannikh nae alikaribishwa keki na mmvinyo
iliyoandaliwa na wanajeshi katika meli. |
|
Balozi
wa Urusi hapa nchini Mheshimiwa Alexander Rannikh akipokea salamu
kutoka kwa kiongozi mkuu Rear Admiral Vladimir Vdovenko wakati
alipotembelea meli hiyo bandarini. |
Wanajeshi wa Kirusi wakionesha umahili wao wa ukakamavu
No comments:
Post a Comment