Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe
(Mb), (Pichani) anatarajiwa kufungua Mkutano wa Kwanza wa Tume ya Pamoja
ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Oman (Joint Permanent
Cooperation), tarehe 24 Februari, 2013 katika Hoteli ya Hyatt Regency
(Kilimanjaro) iliyopo Dar es Salaam.
Mkutano
huo pia utahudhuriwa na Waziri anayeshughulikia Masuala ya Mambo ya Nje
wa Oman, Mhe. Yousuf bin Alawi bin Abdullah anayetarajiwa kuwasili
nchini Jumamosi tarehe 23 Februari, 2013 saa 11 kamili jioni kwenye
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere uliopo mjini Dar es
Salaam.
Mkutano
huo unatokana na Makubaliano yaliyosainiwa tarehe 14 Oktoba 2009 kati
ya nchi hizo mbili mjini Muscat, Oman.
Pamoja
na mambo mengine, Mkutano huo utajadili masuala ya ushirikiano baina ya
Tanzania na Oman katika Sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Nishati na
Madini, Viwanda na Biashara, Elimu, Afya, Uwekezaji, Utamaduni na
Habari.
Imetolewa
na:
KITENGO
CHA MAWASILIANO YA SERIKALI,
WIZARA
YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA,
DAR
ES SALAAM.
No comments:
Post a Comment