TANZANIA YATINGA KWENYE KUMI BORA NDANI YA LONDON FASHION WEEK
=
Wabunifu mitindo Jackline
Kibacha
na Anna Lukindo wakisindikizwa na Mama Balozi Joyce Kallanghe na Mama
Rose Kiondo
Nje ya Jumba la Somerset
Wanamitindo wa Kitanzania
kwenye
London Fashion Week 2013. Anna Lukindo, Christine Mhando, Jacquline
Kibacha
Anna, Jack na Duane kutoka
Jamaica
Anna Luks
Mama Rose Kiondo, Samson Soboye,
Mama Joyce Kallaghe, Anna Lukindo, Christine Mhando, Jacquline Kibacha
Barabara ya The Strand copy
London Fashion Week 2013.Picha zote za Urban Pulse
Imeandikwa na Urban Pulse na Freddy Macha
Jumapili mchana wilaya
ya Westminster jijini London ilikuwa na mashindano ya
ubunifu na
urembo katika maonyesho ya kimataifa ya
London Fashion Week. Mashindano haya yalifanyika jumba
la Somerset lililosimama imara kwenye upembe wa kaskazi
ya mto Thames.
Maonyesho ya
London Fashion Week, bado yanaendelea jumba hili la
Somerset toka tarehe 14 hadi tarehe 28.
Wiki hizi mbili nzima zitakutanisha kila mtu anaye husika na biashara ya
mavazi
na urembo. Magwiji na mapapa wa mitindo, wabunifu, walimbwende, watafuta
vipaji, wafanya biashara, wazalishaji mali ghafi na wamiliki viwanda.
Wote hukutana katika maonyesho haya. Hapa si vipaji
tu vinavyojionyesha, bali pia watu wa biashara.
Siku hii
Tanzania
ilikuwa moja ya nchi mbili tu za Kiafrika zilizochaguliwa na British
Council na
LFW kushiriki kwenye mashindano ya kutafuta
vipaji chipukizi kwenye tasnia ya ubunifu wa mavazi na urembo. Watanzania
Anna Lukindo, Jacqueline Kibacha
na Christine Mhando ndio wasanii
waliobeba bendera ya taifa letu na kutuwakilisha katika mashindano haya
ya
kimataifa yanayofanyika kila mwaka kwa zaidi ya miaka 27 sasa.
Katika kuunga
mkono maendeleo ya Tanzania na Watanzania, Ubalozi wetu
Uingereza na Bodi ya Utalii Tanzania, nao pia walichukua nafasi
hii kuwasaidia
wananchi hawa kufanikisha mahitaji yao ya ushindani. Ubalozi umetoa
Ukumbi wa
Nyumba Ya Tanzania ulioko Bond Street ili wasanii hao waweze kuonyesha
nguo na
sanaa zao kwa juma zima kama sheria za London Fashion Week zinavyoamuru.
Vile vile
Bodi ya Utalii ya Tanzania imesaidia katika mchango wa
mali ghafi zilizotumika katika shughuli
hizi ili kuiuza Tanzania kimataifa.
Mshindi wa tukio
alikua Estonia. Ingawa Tanzania haikuwa
mshindi wa mwanzo- ilichaguliwa kati ya Kumi Bora jambo ambalo
limetikisa nyoyo
na vichwa vya waandaaji,
wabunifu,wafanya biashara na watafuta vipaji vya kimataifa. Hii ni mara
ya
kwanza kwa taifa letu kushiriki katika shughuli na wote
wameguswa na kupumbazwa na usanii wa hali
ya juu ulioonyeshwa na wasanii watatu wa
Kitanzania. Lukindo, Mhando na Kibacha
wamechukua nafasi
waliyopewa kwa mikono miwili na wote wameisogeza Tanzania hatua moja
zaidi
ndani ya ulingo wa kimataifa na katika biashara hii ya mavazi na urembo
ambayo
inasemekana ina thamani ya Pauni Billioni
10 ama
shilingi Trillion 25 za Tanzania.
No comments:
Post a Comment