MAHAKAMA kuu kanda ya Mbeya imewahukumu kunyongwa hadi kufa
watu watatu wakazi wa tukuyu wilayani Rungwe,wakituhumiwa kwa makosa ya mauaji
.
Katika kesi ya kwanza jaji Samweli Karua wamahakama kuu
kanda ya Mbeya iliyohamishia shughuli zake katika mahakama ya wilaya ya
Rungwe,imemtia hatiani na kumhukumu kunyongwa hadi kufa mshtakiwa Rashidi
Mwanyerere baada ya kukutwa na hatia ya kumuua kwa makusudi baba yake mdogo.
Akisoma hukumu Mahakamani hapo Jaji Karua amesema
mhutuhumiwa anatiwa hatiani pasipo shaka kutokana na ushahidi wa mazingira
ambayo mtuhumiwa alimkata na panga marehemu shingoni nakiisha kumwagia maji ya
moto ili kusudi kuzuia damu isimwagike .
Katika kesi ya pili Jaji Kalua amewahukumu kunyongwa hadi
kufa watuhumiwa wawili akiwemo mwanamke kwa kosa la kumbaka kiisha kumuua mtoto
mwenye umri wa miaka mitatu na nusu,watuhumiwa hao ni Mage Kalamu[45]na Ezekia
Nassoro Matatu[43]ambao kwapamoja na kwa makusudi walimuua mtotpo Edina Daudi kwa
kumbaka na kumnyoga shingo.
Watuhumiwa walikutwa na hatia kutokana na majigambo ya
mtuhumiwa wa kwanza Mage Kalamu kwamba pesa zilizo patikana kutokna na kumuua
marehemu zilikuwa ndogo hakuwa nasoko kwani walimuuza kwa shilingi milioni
mbili na nusu.
Kutokana na ushahidi huo Jaji Karua amewahukumu kunyongwa
hadi kufa watuhumiwa wote wawili kutokanana kushindwa kujitetea wala kujibu
lolote mahakamani hapo.
Na SARA ZAKAYO
No comments:
Post a Comment