MRADI wa kutengeneza barabara ya lami kutoka Lwanjilo mpaka
Chunya utaigharimu Serikali ya Tanzania dola za Kimarekani zipatazo milioni 31,
sawa na shilingi bilioni 40.2 za Kitanzania.
Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na meneja mradi wa
kampuni ya ujenzi ya China Communications Construction Company Limited ya
Nchini China, Xia Fei, alipokuwa akizungunza na waandishi wa habari ofisini
kwake katika kijiji cha Chalangwa, wilayani chunya.
Alisema mradi huu
ambao utagharamiwa na serikali ya Tanzania utachukua jumla ya miezi 27
kuumaliza, ambacho ni kipindi cha miaka 2 na miezi 3.
Hata hivyo meneja huyo ame sema kuwa shaka yao kubwa ni
kipindi cha masika ambacho kinakaribia, na ambacho amekielezea kuwa
kitasababisha kazi kuwa ngumu kutokana na mvua.
Alisema kazi imekuwa ikienda taratibu kutokana na serikali
kuchewesha kuwalipa fedha za ujenzi, ambapo aliongeza kuwa fedha zimekuwa
zikitolewa katika mafungu na hivyo kusababisha kazi ya ujenzi kuchelewa kwenda
na wakati.
Fei alisema kuwa awali serikali ilitakiwa kuwalipa asilimia
15 ya fedha zote za ujenzi shilingi bilioni 6.2 za kitanzania, kutoka katika
fedha zote za mradi wa ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 36
ambazo ni shilingi bilioni 40.2.
Alisema badara yake mwanzoni kabisa serikali ilitoa fedha
kidogo ambazo ni bilioni 1.2 zilitolewa Oktoba 2009, na ilipofika Disemba mwaka
huo huo serikali iliongeza fungu linguine la shilingi bilioni 2.23.
Aliongeza kuwa kwa mara ya tatu Juni 2010 serikali ilitoa
tena shilingi bilioni 1.7, na ilipo fika julai mwaka huohuo selikali ilitoa
shilingi bilioni o.841 ili kuendeleza ujenzi wa barabara hiyo.
Meneja mradi huyo alisema kuwa pamoja na kwamba serikali
imetoa maripo kidogo kwa kuchelewesha na bira kufuata mda lakini kampuni yake
ya CCCC wanafanya kazi kwa bidii, ili waweze kumaliza kazi mapema ifikapo
mwakani.
Alisema kuwa mpango nzima na kitu muhimu katika mradi wa barabara
hiyo ni kumaliza ujenzi wa kilomita 36, pamoja na ujenzi wa madaraja makubwa
manne na makaravati zaidi ya 30.
Fei alisema kuwa mpaka sasa kampuni hiyo imekamilisha ujenzi
wa kilomita 11.1 kwa kiwango cha lami na kubakia kilomita 24.9 ambazo
wanatarajia kuzikamilisha mapema mwakani.
Hivi karibuni Waziri wa Ujenzi, John Magufuli alitembelea
eneo la mradi kukagua maendeleo ya ujenzi ambapo aliridhika na kufurahishwa na ubora wa kazi unao fanywa
na kampuni hiyo ya wachina.
Waziri Magufuli aliwapongeza wachina kwa kazi nzuri wanayo
fanya na kuwahimiza kufanya kazi kwa bidii, ili kufikia malengo ya kuimariza
kazi hiyo mapema kabla ya kuikabidhi rasmi kwa serikali.
Hata hivyo waziri huyo wa ujenzi alionya kuwa endapo kampuni
hiyo ya wachina itashindwa kumaliza kazi mapema kamawalivyo kubalina, serikali
haitasita kukatisha mkataba na kuto walipa fedha zao.
No comments:
Post a Comment