ajali

Habari zilizotufikia hivi punde katika chumba cha mbeya leo blog jeshi la Polisi na wasamaria wema wanaendelea kuokoa majeruhi na maiti wa ajali ya gari iliyotokea muda wa masaa mawili yaliyopita kwa kuuhusisha basi la Unique namba za usajili T148 BKK likitokea jijini Mwanza
kwenda Tabora kugongana na lori katika kijiji cha Ibingo kata ya Samuye Shinyanga. 
Akizungumza na Mbeya leo blog, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga, RTO Chacha Marwa alibainisha kuwa, hadi sasa ni watu 10  wamepoteza maisha huku 51, wakijeruhiwa vibaya na kuendelea kukimbizwa hospitali.
“Hadi sasa ni watu 10 wamepoteza maisha. Na tunaendelea kuokoa wengine ambao 51 ni majeruhi. hivyo bado tupo hapa kwa sasa na taarifa zaidi tutaendelea kuzitoa” aliimbi Modewji  RTO Chacha.
Hadi sasa majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.
ajali
Muonekano wa eneo la ajali hiyo kwa picha iliyopigwa kwa mbali.