Wednesday 22 April 2015

PDB YAKIRI KODI ZA BIASHARA SIZIZO RASMI HUISHIA KATIKA MIFUKO YA WATU NA SIO SERIKALI.



Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti ya Vyuo Vikuu vya Afrika ya Kati na Kusini (ESAURP),Profesa Teddy Maliyamkono akifanya mahojiano mafupi na Waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mkutano wa kuwajengea uwezo sekta biashara zisizo rasmi  iliofanyika leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wadau na Wanahabari  wakifuatilia mkutano wa uzinduzi wa mradi wa kuwajengea uwezo wajasiriamali wadogo na wakati kuhuisha biashara zao ili kupata huduma za kibenki iliofanyika leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Ufundi wa FSDT, Sosthenes Kewe alizungumza mbele ya wadau na waandishi wa habari  kuhusiana na uzinduzi wa mradi wa kuwajengea uwezo wajasiriamali wadogo na wakati kuhuisha biashara zao ili kupata huduma za kibenki,Bwa.Kewe amesema kuwa taasisi yake imesaidia mradi huu kwa kuwa unaendana na kazi yao ya kuwezesha wajasiriamali wadogo na wakati na hivyo kuchangia katika kukuza uchumi, kutengeneza ajira na kupanua vyanzo vya kodi.
Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Rais-Ufuatiliaji na Usimamizi wa Miradi (PDB),Omary Issa akifanya mahojiano mafupi na Waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mkutano wa kuwajengea uwezo sekta biashara zisizo rasimi  iliofanyika leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.




ZAIDI ya biashara milioni tatu hazijasajiliwa na mamlaka za utambuzi wa biashara hizo kutokana na kuwa mazingira magumu ya kusajili biashara hizo ikichangiwa na rushwa.

Hayo ameyasema Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Rais-Ufuatiliaji na Usimamizi wa Miradi (PDB),Omary Issa wakati mkutano wa kuwajengea uwezo sekta ya biashara isiyo rasmi,  uliofanyika leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Issa amesema wajasirimali wamekuwa wakilipa kodi lakini zinaishia katika mifuko ya watu na kuisababishia serikali kukosa mapato. Amesema wajasiriamali wakirasimishwa katika mpango huu wataongeza mapato kuliko ilivyo sasa kwa kulipa watu wanaoingiza mifukoni mwao na kuacha serikali kukosa kodi hizo.

Aidha amesema asilimia 40 ya biashara ndogo hazijasajiliwa na mamlaka zinahusika na kufanya wajasiriamali hao kushindwa kupata mikopo katika taasisi za kifedha.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti ya Vyuo Vikuu vya Afrika ya Kati na Kusini (ESAURP),Profesa Teddy Maliyamkono amesema mradi huu wa kurasimimisha biashara utasaidia kukua biashara zao.

Amesema watu wamekuwa wakifanya biashara hazikui kutokana na mitaji yao kuwa midogo na kukosa fursa kukopa katika taasisi za fedha.

No comments: