Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi |
WAFANYABIASHARA Mkoani Mbeya, wameshauriwa kufunga kamera za CCTV katika maeneo yao ya biashara.
Ushauri huo umetolewa leo na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, kutokana na kushamiri kwa vitendo vya uhalifu, vinavyoambatana na wizi wa kutumia silaha
Msangi, amelazimika kulizungumzia hilo, baada ya kutokea kwa tukio la wizi wa silaha, bidhaa na fedha za mauzo lililotokea mwishoni mwa mwezi huu katika moja ya duka lililopo ndani ya Jiji la Mbeya na kwamba uhalifu huo ulifanywa na wanawake.
Amesema kuwa, wanawake hao ambao ni mama lishe waliingia ndani ya duka moja lililopo Jijini hapa na kufanikiwa kuiba bastola moja na mali kisha kukimbia, lakini kamera za CCTV zilizofungwa ndani ya duka hilo ziliweza kuwanasa.
Hata hivyo,Msangi amesema kuwa polisi inawatafuta watuhumiwa hao kwani baada ya kubaini kuwa wanatafutwa walitelekeza bastora hiyo kutoroka, mbali na kufanya uhalifu kwenye duka hilo pia wamewaliza watu wengi.
No comments:
Post a Comment