Kamanda wa Polisi wa kikosi cha usalama Barabarani Mohammed Mpinga,akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano na Kamanda wa Polisi wa kikosi cha usalama barabarani Mohammed Mpinga
KIKOSI cha Usalama Barabarani kimesema wanazifuta leseni zote kwa madereva waliosababisha ajali kwa uzembe zikiwemo ajali za hivi karibuni.
Hayo ameyasema jana jijini Dar es Salaam,Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani,Mohamed Mpinga,amesema katika kukabiliana na wimbi la ajali ni pamoja na kufuta leseni kwa madereva wazembe ambao wanasababisha ajali.
Mpinga amesema ajali za hivi karibuni zimesababishwa na uzembe wa madereva, hivyo ni lazima kufuta leseni zao na hawatakiwi kufanya kazi yoyote ya udereva nchini pamoja na kuweka katika tovuti taarifa zao ili watu wengine wasiwachukue.
Amesema katika usafiri wa mabasi watakuwa wanaangalia muda kutoka sehemu hadi nyingine na basi ambalo litakuwa mbele ya muda uliopangwa katika eneo husika hatua zitachukuliwa.
Mpinga ametoa pole kwa wafiwa waliopoteza maisha katika ajali za hivi karibuni na kusema wale wote waliosababisha ajali hizo watafutiwa leseni na hatua zingine kufuta ili madereva wengine wasifanye makosa hayo.
No comments:
Post a Comment