TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 21.04.2015.
· KIJANA WA MIAKA 20 AUAWA KWA KUPIGWA NA WANANCHI KWA TUHUMA ZA WIZI MKOANI MBEYA.
· MWANAMKE AMUUWA MUME WAKE KWA KUMCHOMA KISU KIFUANI KUTOKANA NA WIVU WA KIMAPENZI.
· JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA LINAMSHIKILIA KIJANA MMOJA AKIWA NA NOTI BANDIA ZIPATAZO 65.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
KIJANA MWENYE UMRI WA MIAKA 20 ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA FADHIL SIKAPUNDWA, MKAZI WA NAMTAMBALALA WILAYANI MOMBA ALIUAWA PORINI KWA KUPIGWA FIMBO SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA WATUHUMIWA WALIOTAMBULIKA KWA MAJINA YA 1. SHADRACK SIMBEYE (16) 2. JOB JOHN (21) NA 3. MASUOD SIMWAKA (18) WOTE WAKAZI WA NAMTAMBALALA WILAYANI MOMBA.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 19.04.2015 MAJIRA YA SAA 19:00 JIONI HUKO KATIKA KIJIJI CHA NAMTAMBALALA, KATA YA NZOKA, TARAFA YA NDALAMBO, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA, CHANZO CHA TUKIO HILO NI TUHUMA ZA WIZI WA VIATU, SIMU NA NGUO. WATUHUMIWA WAMEKAMATWA NA UCHUNGUZI ZAIDI WA TUKIO HILI UNAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGIANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI KUFANYA HIVYO NI KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAJENGE TABIA YA KUWAFIKISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA WATUHUMIWA WANAOKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MWANAMKE MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA IYENGA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA PILLY MGALA ALIMUUAMUME WAKE AITWAYE AMADI MWASHAMBWA, (42) MKAZI WA KIJIJI CHA IYENGA KWA KUMCHOMWA KISU KIFUANI.
AWALI MNAMO TAREHE 19.04.2015 MAJIRA YA SAA 21:00 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA IYENGA, KATA YA ISANSA, TARAFA YA IGAMBA, WILAYA YA MBOZI MWANAMKE HUYO ALIMJERUHI MUME WAKE KWA KUMCHOMA KISU KIFUANI NA KUPELEKEA KUKIMBIZWA KATIKA ZAHANATI YA KIJIJI CHA IYENGA KWA MATIBABU. KUTOKANA NA MAJERAHA ALIYOYAPATA MNAMO TAREHE 20.04.2015 MAJIRA YA SAA 13:00 MCHANA ALIFARIKI DUNIA WAKATI ANAPATIWA MATIBABU.
CHANZO CHA TUKIO HILO NI UGOMVI ULIOTOKANA NA WIVU WA KIMAPENZI BAADA YA MAREHEMU KUMTUHUMU MKE WAKE KUWA SIO MWAMINIFU KATIKA NDOA YAO. MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO NA MSAKO MKALI UNAENDELEA WA KUMTAFUTA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGIANATOA WITO KWA WANANDOA KUTATUA MIGOGORO YAO KWA KUKAA MEZA MOJA NA KUFIKIA SULUHISHO ILI KUEPUKA VITENDO VYA KUJICHUKULIA SHERIA VINAVYOWEZA KUSABABISHA MADHARA NA MATUKIO KAMA HAYA YA MAUAJI.
TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA KIJANA MMOJA MKAZI WA FOREST YA ZAMANI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA EMANUEL SAMWEL (28) AKIWA NA NOTI BANDIA AMBAZO KAMA ZINGEKUWA HALALI ZINGEKUWA NA THAMANI YA TSHS 325,000/=.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 20.04.2015 MAJIRA YA SAA 16:00 JIONI HUKO ENEO LA ISYESYE, KATA YA ISYESYE, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA MBEYA AKIWA KWENYE HARAKATI ZA KUJARIBU KUWEKA PESA HIZO KWENYE AKAUNTI YAKE YA TIGO-PESA KWENYE DUKA LA MARY PATRICK (32) MFANYABIASHARA NA MKAZI WA ISYESYE.
NOTI HIZO ZILIKUWA NA NAMBA DT. 2937833 NOTI 6, BV 2937839 NOTI 10, DT 4243042 NOTI 4, BF 1547948 NOTI 5, BV 4243044 NOTI 8, AA 4243045 NOTI 18, DT 1547949 NOTI 5 NA BC 2937831 NOTI 10. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGIANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA PINDI WAONAPO VIASHIRIA VYA UHALIFU AU WANAPOMTUHUMU MTU/WATU ILI HATUA STAHIKI ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment