Friday, 17 April 2015

Membe: Watanzania wengine 64 kuondoshwa Yemen


Membe: Watanzania wengine 64 kuondoshwa Yemen
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya Tanzania amesema kuwa, Watanzania 64 walioko nchini Yemen watarejeshwa nchini humo hivi karibuni ili kuwaepusha na machafuko yanayoendelea nchini humo.

 Bernard Membe ambaye yuko nchino Oman kwa ziara ya siku moja na alizungumza na Balozi wa Tanzania nchini humo, Ali Ahmed Saleh, na kusema serikali ina jukumu la kuhakikisha usalama wa raia wake.

“Nimeruhusu matumizi ya fedha ya dharura ili kuhakikisha ndugu zetu walioko kwenye hatari na machafuko huko Yemen wanarejeshwa salama nyumbani mara moja,” alisema Membe.

 Alisema raia hao ambao wengi ni wanafunzi, watarejea nchini salama na hiyo ni kufuatia kupewa kwao ruhusa ya kuingia nchini Oman. Siku chache zilizopita, watanzania 25, walirudishwa nchini kutoka Yemen chini ya utaratibu wa Ofisi za Ubalozi wa Tanzania mjini Muscut, Oman, na sasa awamu hii watarudishwa raia 64. Taarifa hiyo pia ilisema, hivi sasa wanafunzi hao wamefika kwenye mji wa Sarfat na Al-Mazyouna iliyopo mpakani mwa Oman na Yemen.

No comments: