Wednesday, 6 May 2015

BURUNDI: MGOMBEA URAIS AKAMATWA NA BAADAYE AACHILIWA HURU

Audifax Ndabitoreye amekamatwa alipokua akiondoka katika hoteli Panoramique ambapo kulikua kukifanyika mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje kutoka jumuyiya ya Afrika Mashariki (EAC), Mei 6 mwaka 2015.
Audifax Ndabitoreye amekamatwa alipokua akiondoka katika hoteli Panoramique ambapo kulikua kukifanyika mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje kutoka jumuyiya ya Afrika Mashariki (EAC), Mei 6 mwaka 2015.
Na RFI
Kwa muda wa masaa kadhaa akiwa mikononi mwa polisi, Audifax Ndabitoreye, ambaye hivi karibuni alitangaza kuwania katika kinyanga'nyiro cha urais katika uchaguzi ujao wa urais, ameachiliwa huru.

Audifax Ndabitoreye, alishiriki mara kadhaa katika maandamano yanayoendelea kushuhudiwa jijini Bujumbura. Mkuu huyo wa zamani wa Idara ya Ujasusi amekamatwa na polisi Jumatato saa kumi na mbili jioni wiki hii, akituhumiwa na utawala kuanzisha vurugu katika mji wa Bujumbura.(P.T)
Audifax Ndabitoreye alikamatwa baada ya kushiriki mkutano wa mawaziri wa mashauri ya kigeni kutoka jumuiya ya Afrika Mashariki, ambao wamejielekeza Jumatano wiki hii mjini Bujumbura kukutana kwa mazungumzo na viongozi wa nchi ya Burundi, hususan rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza pamoja na wadau wote katika suala nzima la mchako wa uchaguzi katika hali ya kutafutia suluhu maandamamno yanayoendelea, na kuepuka vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.
Hata hivyo kabla ya mkutano huo, waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Bernard Membe, aliwaahidi viongozi wa vyama vya upinzani na wale wote watakaoshiriki mkutano huo kwamba hawatokamtwa wala kufanyiwa vitisho.
Akizungumza na RFI, Jumatano usiku, Audifax Ndabitoreye amehakikisha kuwa yuko na mkewe nyumbani kwake, licha ya kupata maaumivu kwenye goti baada ya kudondoka kutoka katika gari alilokuwemo kutokana na mlango wa gari ambao haukua umefungwa vizuri.
Mawaziri hao wa mashauri ya kigeni kutoka jumuiya ya Afrika Mashariki wamefahamisha kwamba wamekwenda Burundi kuandaa mkutano wa marais wa nchi kutoka jumuiya hiyo, mkutano ambao umepangwa kufanyika Jumatano Mei 13.
Itafahamika kwamba mawaziri hao wameondoka mjini Bujumbura Jumatano jioni wiki hii.
Hayo yakijri maandamano yameendelea kushuhudiwa jijini Bujumbura kwa siku ya 10. Maandamanao hayo pia yamefanyika katika mikoa ya Bujumbura, Mwaro na Muramvya. Mpaka sasa zaidi ya wakimbizi 60,000 kutoka Burundi wameikimbia nchi yao. Rwanda imewapa hifadhi zaidi ya wakimbizi 40,000, Tanzania mpaka sasa imewapokea wakimbizi 11,000, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imewapakoa wakimbizi zaidi ya 4000, kulingana na idadi iliyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi.

No comments: