Wednesday, 6 May 2015

Watanzania 53 wamewasili wakitokea nchini Yemen,na kuishukuru serikali ya Tanzania kuwawezesha kurejea nyumbani Salama.


Jumla ya watanzania 53 wamewasili nchini wakitokea nchini Yemen,na kuishukuru serikali ya Tanzania kwa kuwawezesha kurejea nyumbani wakiwa salama,kufuatia nchi waliyokuwa wakiishi ya Yemen kukumbwa na machafuko ya kivita ya wenyewe kwa wenyewe na hivyo kuhatraisha usalama wa maisha yao.

Wakiongea kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar-es-salaam,wananchi hao wamesema kuwa,wamerejea nchini mara baada ya wito wa serikali ya jamuhuri ya muungano ya Tanzania,kuwataka raia wote wealiopo nchini Yemen kujisalimisha kwenye balozi za karibu nchi za uarabuni ili warejeeshwe nyumbani.
 
Akiongea kwa niaba ya serikali ya jamuhuri ya mungano wa Tanzania,msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa bwana Ally Mkumbo,amewaomba watanzania waishio na kusafiri kwenda nchi za nje,kujiandikisha kwenye balozi za nchi husika,ili kutambulika na kupata msaada mara anapopata tatizo.
 
Mpaka sasa jumla ya watanzania 71 wamekwisha wasili kutoka nchini Yemen,kwa kusafirishwa na serikali ya jamuhuri ya mungano wa Tanzania pamoja na shirika la kimataifa la wahamiaji IMO,ambapo watanzania hao walianzia safari zao katika nchi za JEDDA wakiwa 14 na MASCAT OMANI wakiwa 39,ambapo msemaji wa shirika hilo amesema, wataendelea kusafirisha watanzania zaidi walipo katika nchi mbalimbali wanaohitaji msaada huo.
 

No comments: