Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akifafanua
jambo mbele ya waandishi wa Habari leo (hawapo pichani) ,jijini Dar es
Salaam, kuhusiana na kubadilika kwa tarehe ya mkutano wao kufuatia
kuingiliana na Mkutano wa Baraza la Wawakilishi.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye Akizungumza
na waandishi wa Habari leo ,jijini Dar es Salaam, kuhusiana na
kubadilika kwa tarehe ya mkutano wao kufuatia kuingiliana na Mkutano wa
Baraza la Wawakilishi.
========= ======== =======
Chama
cha Mapinduzi (CCM),kinatarajia kufanya vikao vyake mjini Dodoma,ambapo
Mei 22 kitafanyika kikao cha kamati kuu ya CCM,na kufuatia kikao cha
Halmashauri kuu ya CCM Taifa kitachofanyika Mei 23 na 24-2015 mjini
Dodoma.
Akizungumza
na waandishi wa Habari ,jijini Dar es Salaam,Katibu wa NEC, Itikadi na
Uenezi,Ndugu Nape Nnauye amesema kuwa kubadilika kwa siku za mikutano
hiyo kunatokana na kuingiliana na Mkutano wa Baraza la Wawakilishi.
Nape
amesema vikao vyote vikubwa vitafanyika mkoani Dodoma,ambapo ajenda
mbalimbali zitatolewa ikiwa ni pamoja na maoni ya Ilani ya CCM 2015-2020
ambayo itawasilishwa na Kamati iliyoundwa kwa kazi hiyo.
Amesema
kutakuwa na vikao vya kawaida Mei 21 hadi 22 ambavyo vitakuwa
vinafanyika mkoani Dodoma na Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya
Mkutano wa Kamati kuu ya CC na Halmashauri Kuu (NEC).
Nape amesema vikao hivyo vitaongozwa na Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Kikwete katika kujadili masuala mbalimbali ikiwemo hali ya siasa ya chama hicho.
Wakati huo huo Nape amesema
kuwa wanachama sita waliofungiwa bado hatma yake kutokana na suala
hilo linashughulikiwa na kamati mbili ambazo ndizo zinaweza kusema
kifungo kinaendelea ama la,amesema na kuongeza kuwa Chama cha
Mapinduzi (CCM) kinaongozwa na kanuni ambazo yeye mwenyewe amezikuta
hivyo ni lazima wanachama na makada wazifuate kanuni na miongozo ya
chama.
Amesema
wanachama kutangaza nia ya kugombea sio tatizo lakini mazingira
yanayoendana baada ya kutangaza nia hiyo ndipo kanuni na miongozo ya
chama inaanza kutumika,amesema kanuni na miongozo ya CCM zinasema
mtu ambaye yuko kwenye kifungo katika chama haruhusiwi kugombea nafasi
yeyote ndani ya chama ambazo zipo wazi.
Amesema
mikutano hiyo itajadili jinsi gani watu watapochukua fomu,urudishaji wa
fomu pamoja na njia ambazo zitatumika katika utangazaji nia kwa
wagombea kutokana na mazingira yaliyopo.
No comments:
Post a Comment